Na Lucas Raphael,Tabora
Mbunge wa jimbo la Igalula wilaya ya uyui mkoani Tabora Venant Protas amekusudia kutekeleza mpango wa kuanzisha ligi ya wilaya hyo itakayohusisha timu za wilaya nzima ya Uyui hatua ambayo itasaidia kuongeza kasi ya kuibua vipaji kwa vijana hususani waishio vijiji ambao wamekuwa wakisahaulika.
Alitoa kauli hiyo Octoba 31, 2022 alipokuwa akikabidhi vifaa vya michezo katika kata ya kigwa zoezi ambalo amekuwa akilitekeleza katika vijiji 58 vya jimbo la Igalula kama hamasa kwa vijana kupenda michezo.
Alisema kuwa wanamichezo wote katika wilaya hiyo kuendelea kujifua kwa ajili mandalizi ya ligi ya wilaya ambayo anakusudia kuanzisha hivi karibuni.
Venant alisema michezo ni ajira michzo inadumisha umoja na mshikamano miongoni mwa vijana wa kata moja na kata nyingne.
Alisema umoja kwa wanamichezo ni nguzo muhimu kwa vijana ambao wanatarajia kushiri ligi ya wilaya ya uyui na kuhakikishia vijana hao kuifanya ligi hiyo kuwa bora miongoni mwa ligi katika mkoa wa Tabora.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui, Said Ntahondi alipongeza hatua hiyo ambayo inakwenda kuwa chachu katika kukuza na kuibua vipaji vya soka hapa nchini na kuwataka wadau wengine kuendelea kuwapiga tafu vijana hasa walioko vijijini.
Alisema kwamba kuibua kwa vipaji vya wanamichezo vijijini kutasaidia kupatikana kwa wanamichezo waliobora wa miaka ijayo .
“Mbunge leo unaona umefanya jambo hili la kutoa vifaa vya michezo kwenye kata 58 lakini jambo ili sio ndogo hata kidogo bali likifanyika kwa kila kata litaibua vipaji vilivyo bora na hivyo wilaya ya uyui itatoa samata wa miaka ijayo “alisema Ntahondi
Mwisho