Wahalifu wamevamia kituo cha polisi cha Kipasi na kuiba bunduki na risasi kadhaa na kisha kuingia mafichoni.
Bado haijabainika ni vipi kisa hicho kilifanyika ndani ya kituo cha polisi ambapo kwa kawaida usalama huwa ni mkali.
Polisi katika kituo hicho kilicho eneo bunge la Mbita nchini Kenya walisema wezi hao walivamia eneo ambapo silaha huwekwa.
Waligundua baadaye kuwa bunduki nne pamoja na ngunia la risasi 110 zilikuwa zimetoweka na hivyo kuanza msako.
Mkuu wa polisi katika eneo la Homa Bay Samson Kinne amedhibitisha kisa hicho huku akisema uchunguzi unaendeshwa kuhakikisha wahusika wamekamatwa.
Kinne ameongeza kuwa kisa hicho kimezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wananchi wanaohisi kuwa usalama wao umo hatarini kutokana na kuibwa kwa silaha hizo.
Wanahoji ni vipi majambazi wanaweza kuwa na ukakamavu wa kuingia katika kituo cha polisi ambacho ulinzi huwa mkali. Cc Tuko