Timu ya wataalam wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) leo Novemba 11 , 2022 imeendelea kukusanya taarifa za uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ya uchimbaji madini kwa lengo la kuandaa ramani maalum itakayoonesha aina za madini mbalimbali katika Mkoa wa kimadini Mahenge kama ilivyoagizwa na Waziri mwenye dhamana Katika sekta ya Madini nchini.
Ramani na taarifa za uwepo wa madini itatumika kuvutia uwekezaji ndani ya Wilaya ya Mahenge/Ulanga.