Breaking

Sunday, 13 November 2022

BRELA WATOA HUDUMA ZA PAPO KWA PAPO MAONESHO YA BIASHARA YA KKKT




Maafisa kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakitoa huduma za papo kwa papo kwa wadau walio tembelea katika Maonesho ya kwanza ya Biashara ya Kanisala Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Temboni, wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam.

Katika Maonesho hayo mbali na kutoa huduma za usajili wa majina ya biashara na kampuni pia BRELA inawapatia elimu wadau wanaotembelea banda hilo, kuhusu huduma zote zinazotolewa na Taasisi.




Maonesho hayo yanayoratibiwa na Benki ya Maendeleo yanafanyika tarehe 12 na 13 Novemba, 2022.











Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages