Breaking

Thursday 3 November 2022

BODABODA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI GEITA




Amini Salum (30), mkazi wa mtaa wa Nyamalembo Halmashauri ya mji Geita amefariki dunia kwa kupigwa Risasi na majambazi baada ya kumsaidia mtu aliyekuwa anataka kuvamiwa na majambazi hao.

Tukio hilo limetokea Alfajiri ya Novemba 1/2022 ambapo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwakamata wote wakiohusika na shambulio hilo.

"Ni tukio la kusikitisha ambapo majambazi, walitaka kujaribu kumpora mfanyabiashara mmoja ambae jina lake linahifadhiwa, na kwa bahati nzuri, yule mwananchi akaweza kukimbia na akapata msaada wa bodaboda, baada ya kupata msaada wa bodaboda, wale bodaboda sasa kwa kushirikiana na yule mhanga, wakaanza kuwafukuza wale majambazi, kwa bahati mbaya wale majamabazi walikuwa na silaha wakamfyatulia yule bodaboda" amesema Kamanda Jongo

Marehemu ameacha mke na watoto watatu

Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages