Polisi katika jimbo la Florida nchini Marekani wamemkamata Bi. Harusi mmoja na kiongozi wake wa mapishi kwa tuhuma za kuongeza bangi katika chakula cha wageni katika harusi hiyo.
Kukamatwa kwao kunajiri miezi miwili baada ya maafisa kuitwa katika harusi hiyo kusaidia wageni waliosema kuwa walikuwa wakihisi kanakwamba wamelishwa dawa za kulevya.
Danya Svoboda na mkuu wake wa mapishi Joycelyn Bryan wanakabiliwa na mashtaka ya kuhitilafiana, utepetevu na kutia bangi katika chakula cha watu.
Maafisa wa polisi waliwakamata wawili hao baada ya kufanyia vipimo vyakula na vinywaji katika harusi hiyo iliyofanyika Februari 19 katika jiji la Longwood jimbo la Florida.
Wageni walitapika na kuumwa na tumbo Wageni wlaikuwa watapika na kulalamikia maumivu ya tumbo, wengine wakipelekwa hospitalini kwa matibabu baada ya kuzidiwa.
Kwa mujibu wa maafisa, Bi. Harusi aliulizwa na polisi katika harusi hiyo iwapo alikuwa ameruhusu dawa kuwekwa kwa chakula lakini akakana.
Mmoja wa wageni kwa jina Miranda Cady alisema kuwa alimuona mmoja wa wapishi akiongeza kiungo cha majani katika chakula.
Cady alidai kuwa Bi. Harusi alikiri kuongeza bangi katika mafuta ya mzeituni maarufu kama Olive oil wakiwa katika ukumbi wakisakata densi.
Kiongozi wa mapishi na wafanyakazi wake waliondoka katika harusi hiyo kabla ya kujohiwa na polisi ambao walichukua baadhi ya vyakula na vinywaji kwa ajili ya vipimo.
Maafisa wanasema kwamba vipimo viliashiria baadhi ya vyakula kama vile mkate viliashiria kutiwa bangi na wawili hao kukamatwa.
Japokuwa bangi ni halali katika jimbo la Florida, ni hatia kuitumia kujivinjari.
Via: Tuko