Breaking

Sunday, 23 October 2022

WATUMISHI BRELA WAFUNDWA JUU YA VVU, MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA



Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamepata mafunzo Kuhusu Virusi vya UKIMWI na magojwa yasiyoambukiza katika Chuo Cha Utalii Jijini Dar es salaam.

Mafunzo hayo yametolewa 
Oktoba 22, 2022 na wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambao ni Dkt. Alice Temu, Dkt . Vaileth Ndosi pamoja na Daktari Bingwa wa Magojwa ya akili Dkt. Garvin Kweka.



Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea watumishi uelewa kuhusu afya zao pamoja na kujiepusha na magonjwa mabilmbali yanayoambukiza na yasiyoambukiza ambayo yasipodhibitiwa yanaweza kuathiri utendaji kazi kwa watumishi.

Mbali na mafunzo ya afya pia watumishi hao wamepata elimu ya masuala ya kifedha na fursa za mikopo kutoka kwa maafisa wa ya Standard chartered pamoja na elimu ya Bima kutoka Maafisa wa Shirika la Bima la Taifa(NIC).



BRELA imekuwa ikifanya mafunzo mbalimbali ya kuwaongezea ujuzi na ufanisi mahala pazi ili kuleta matokeo chanya kwa wadau inaowahudumia na jamii kwa ujumla.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages