Walimu 13 wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wamefukuzwa kazi kutokana na makosa ya utoro huku wengine wanne wakiendelea kujadiliwa kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo kujihusisha na mapenzi na wanafunzi pamoja na ulevi uliopindukia katika kipindi cha miaka miwili kuanzia 2020 hadi Septemba.
Katibu wa tume ya utumishi wilayani humo Fedinand Ndomba amesema tabia ya utoro inayofanywa na baadhi ya walimu imekua ikichangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi hivyo uamuzi wa kuwafuta kazi walimu hao ni ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa Pwani Douglas Mhini ameeleza changamoto zinazowakabili walimu ikiwemo kucheleweshwa kwa fedha za uhamisho pamoja na malipo kwa wastaafu.
Nae katibu tawala wilaya ya Bagamoyo Kasilda Mgeni akimuwakilisha mkuu wa wilaya amekemea vitendo viovu vinavyofanywa na walimu na kamwe hatovifumbia macho vitendo hivyo.
Via : EATV