Breaking

Wednesday, 26 October 2022

“TUTUNZE NA KUHIFADHI MAZINGIRA ILI YATUTUNZE” NAIBU WAZIRI MASANJA




Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amewataka wananchi wa eneo la Ubaruku Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya kuendelea kutunza na kuhifadhi mazingira ili waendelee kufaidika na uwepo wa mvua na hali ya hewa nzuri.

Ameyasema hayo leo katika Ziara ya Kamati ya Mawaziri wa Kisekta Mkoani Mbeya.


“Tunapoharibu maeneo ya Hifadhi na mazingira tunasababisha mvua zisije” amesisitiza.

Naibu Waziri Masanja amefafanua kuwa wananchi wamevamia maeneo ya Hifadhi na kufanya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji akitolea mfano wa uvamizi katika Mto Ruaha.

Amewaasa wananchi kuacha uvamizi katika maeneo ya hifadhi ili kuondokana na uharibifu wa vyanzo vya maji, ukataji miti na uchomaji mkaa na hatimaye kurithisha vizazi vijavyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages