Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Kupitia taarifa iliyotolewa leo Alhamisi Oktoba 20, 2022 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Prof. Aboud ni Profesa Mshiriki, Mhadhiri Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.
Prof. Aboud anachukua nafasi ya Prof. Yunus Daud Mgaya ambaye amemaliza muda wake mwezi Septemba, 2022.
Taarifa imeeleza kuwa Uteuzi huo umeanza tarehe 19 Oktoba, 2022.