Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 10 katika mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar (Jina linahifadhiwa) anadaiwa kumuingilia mtoto wakike mwenye umri wa miaka 2.
Mama wa mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho amedai kuwa aligundua tukio hilo wakati akimuogesha mtoto wake na alipomuuliza nani amefanya kitendon hicho alimtaja mtoto mwenzake kuwa anahusika
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Richard Thadeo Mchomnvu ameitaka jamii kuishi katika mila na desturi na kuwalea watoto katika misingi ya dini ili kuepuka matukio kama hayo.
VIA: EATV