Breaking

Saturday, 22 October 2022

MOTO WAZUKA MLIMA KILIMANJARO



Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umezuka katika mlima Kilimanjaro, karibu na eneo la Karanga Camp lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka na jitihada ya kuuzima zinaendelea.


Moto huo ulianza kuonekana jana Ijumaa Oktoba 21, 2022 usiku kutokea Moshi Mjini, ambapo Kamishina wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi Tanzania (Tanapa), William Mwakilema aliyezungumza na Mwananchi leo Oktoba 22, amesema vikosi vinaelekea kuuzima moto huo.


Taarifa zinaeleza moto huo unawaka ukanda wa Moorland, ambao mimea yake ikishika moto huwa ni mkali na tayari Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) na Hifadhi ya Kilimanjaro (Kinapa) wametuma vikosi kwenda kuukabili.


Akizungumza kwa simu na Mwananchi jana Oktoba 21, Kamishina wa Uhifadhi kanda ya Kaskazini, Betrita James amesema baada ya kupata taarifa za kuonekana kwa moto huo, menejimenti ya Kinapa ilianza mara kazi ya kukusanya nguvu kazi na vifaa, na tayari timu zimeelekea eneo hilo.


Mmoja wa waongoza watalii mwenye uzoefu na njia hiyo, Geness Shirima, amesema kwa kadri alivyojulishwa, moto huo uko karibu na Karanga Camp na Askari wa Kinapa na wadau wengine walikuwa wakielekea huko kushiriki kazi ya kuuzima.


Via: Mwanachi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages