Breaking

Thursday, 27 October 2022

BODABODA AUAWA, MWILI WATUPWA PORINI




Kijana Bakari Yasini (18) mkazi wa Kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara, ameuawa na mwili wake kutupwa pori la Lengati Kata Njoro.

Yasini ambaye alikuwa ni dereva bodaboda mjini Kibaya alitoweka Oktoba 21.2022 baada ya kukodishwa na mtu asiyejulikana usiku wa saa tatu na nusu na kutoweka kusikojulikana.

Taarifa kutoka kwa wenzake aliowaaga baada ya kukodishwa na mtu huyo zinaeleza kuwa amekodishwa kuelekea Kijiji cha Olpopong na hakurejea hadi alipopatikana akiwa amefariki dunia.

Ilielezwa ndugu jamaa na marafiki baada ya kutorejea walitoa taarifa Kituo cha Polisi Kibaya ambapo walishirikiana pamoja kumtafuta.

"Jeshi la Polisi Kiteto tulipata taarifa za kupotea kwa dereva huyo, Bakari Yasini (18) Oktoba 21.2022 jitihada za kumtafuta ziliendelea hadi alipopatikana jana Oktoba 26.2022" alisema Kamanda wa Mkoa wa Manyara George Katabazi.

Alisema kupatikana kwa marehemu huyo kumetokana na jitihada kubwa zilizofanywa kwa ushirikiano wa wananchi ambapo amewataka waendelee kutoa ushirikiano huo kwa Polisi mara yanapotekea matukio kama hayo.


Via Mwanachi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages