Mwanamke mwenye umri wa kati kutoka kaunti ya Meru, alinusurika kifo kwenye tundu ya sindano Jumanne, Oktoba 25, baada ya wakazi wenye hasira kumvamia nyumbani kwake akidaiwa kufumaniwa akifanya mapenzi na mwanawe wa kiume.
Mwanamke huyo kutoka Kiguchwa eneo la Tigania ya Kati alikabiliwa na ghadhabu za wanawake wenzake baada ya kuripotiwa kuwa katika mahusiano ya karibu na mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 27.
Kulingana na chifu wa eneo hilo Edwin Mwiti, mwanamke huyo anadaiwa kuwa na tabia ya kuwavizia wavulana wadogo na mwanawe kufanya naye tendo la ndoa, hatua aliyosema iliwakera wanakijiji waliotaka kuangamiza maisha yake.
"Nimepokea ripoti kwamba mwanamke huyo alifumaniwa mumewe akifanya tendo hilo na mwanawe na ambaye alipiga nduru iliyowavutia wanakijiji," chifu huyo alisema kama alivyonukuliwa na K24.
Aliongeza kuwa wenyeji waliamua kufuata sheria za kimila kumwadhibu mwanamke huyo ambaye walimtaja kama mtu hatari kwa wavulana wadogo na wanaume katika eneo hilo. Kisha baadaye alitolewa nje ya nyumba yake na wanawake wenzake wenye hasira baada ya mumewe kuwajuza habari hizo.
Umati wa watu ulivamia boma la mwanamke huyo katika kijiji cha Kanguba huku wakiimba nyimbo na kubeba matawi kabla ya kumburuta hadi kwenye kituo cha soko lilo karibu.
Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina Kaumi alilazimishwa kubeba ndizi mbivu mgongoni huku wanawake wenzake wakimpiga mijeledi
Mamlaka ya eneo hilo pia ililaani kitendo hicho ikisisitiza kuwa mwanamke huyo na mwanawe wanapaswa kukabiliwa kisheria.