Breaking

Sunday, 23 October 2022

WAZIRI BASHUNGWA AHIMIZA UTUNZAJI UOTO WA ASILI NA MISITU




Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Watanzania kutunza uoto wa asili na misitu iliyopo nchini na kujenga tabia na msukumo binafsi wa kupanda miti.


Ametoa wito huo Oktoba 22, 2022 wakati alipotembelea makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Chamwino, Jijini Dodoma.


"Tutunze uoto wa asili na misitu iliyopo na kujenga tabia na msukumo binafsi wa kupanda miti kwenye makazi, mahali pa kazi, mashambani, mjini na vijijini" amesisitiza Waziri Bashungwa


Bashungwa amesema Uhai na ustawi wa mwanadamu na viumbe vyote hapa duniani (ecosystem) vinategemea faida lukuki tunazozipata kutoka kwenye miti na misitu.


Aidha, Bashungwa amesisitiza Uzalendo na kufafanua kuwa ni utayari wa kutetea na kulinda ustawi wa Taifa letu la Tanzania, masilahi yake pamoja na watu wake.


Wakati huo, Bashungwa amelipongea Jeshi la Kujenga Taifa kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na malezi ya vijana, uzalishaji mali kupitia SUMAJKT na ujenzi wa miradi mikubwa ya kitaifa.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages