Breaking

Saturday, 8 October 2022

MTOTO WA MIAKA 13 ADAIWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA MIWILI




Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia mtoto wa miaka 13 mkazi wa kijiji cha Minyembe halmashauri ya Wilaya ya Mtwara kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka miwili.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema tukio hilo lilitokea Septemba 30, 2022.

Amesema mtuhumiwa anashikiliwa na polisi akisubiri uchunguzi ukamilike ili afikishwe mahakamani.

“Jeshi linakemea ukatili wa aina hiyo dhidi ya watoto, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote wanaoendelea kufanya ukatili kama huo,” amesema Katembo.


Source: Mwanachi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages