Breaking

Friday, 28 October 2022

DKT. BITEKO ASISITIZA UTEKELEZAJI MAKUBALIANO KATI YA TANZANIA NA BURUNDI KUHUSU USHIRIKIANO SEKTA YA MADINI




Waziri wa Madini nchini Dkt. Doto Biteko amesisitiza kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Makubaliano baina ya nchi ya Tanzania na Burundi katika kubadilishana ujuzi wa mnyororo mzima wa Sekta ya Madini nchini.

Dkt.Biteko ameyasema hayo Leo Oktoba 28, 2022 mkoani Dodoma alipokutana na ujumbe maalum kutoka Jamhuri ya Burundi katika hafla ya kuuaga ujumbe huo baada ya kumaliza ziara ya siku sita nchini ya kujifunza kuhusu usimamizi na maendeleo ya Sekta ya Madini nchini.

Dkt.Biteko ameendelea kuushukuru ujumbe huo na kusema kuwa amefurahishwa na ugeni huo na anaamini kuwa yote yaliyokubaliana nayo yatafanyika kwa ushirikiano kwa lengo la kupanua mipaka ya ushirikiano Katika sekta ya Madini.

Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe huo ambaye pia ni mshauri wa Rais Katika masuala ya Madini nchini Burundi Alphonsia Kwizera , ameipongeza serikali ya Tanzania kuwa na sera nzuri za kuiendeleza Sekta ya Madini na usimamizi mzuri wa sekta ya madini kwa wachimbaji wadogo na wa kati.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wizara ya Madini Adolf Ndunguru amepongeza ujumbe huo na kutumia siku zote sita walizotumia kujifunza masuala ya Sekta ya Madini nchini na kufafanua kuwa kujifunza hakuna mwisho hivyo Tanzania na Burundi zitaendelea kubadilishana uzoefu kwasababu maswala ya kupeana ujuzi ni makubaliano ya pande mbili

Ziara hii ni matokeo baada ya Tanzania na Burundi kusaini makubaliano juu ya ushirikiano Katika usimamizi wa rasilimali madini.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages