Breaking

Sunday, 16 October 2022

JESHI LA POLISI KUICHUNGUZA KALYNDA




Jeshi la Polisi nchini limeanza kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya wananchi kutapeliwa fedha zao na kampuni ya Kalynda e Commerce.

Kupitia taarifa iliyotolewa Oktoba 15, 2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imeeleza kuwa Ofisi Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza malalamiko hayo ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa.

“Kutokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi kulalamika kutapeliwa fedha zao na kampuni waliyoeleza ni Kalynda E Commerce kwa njia ya mtandao, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai kwa kushiriana na taasisi nyingine za kiuchunguzi na za kifedha wameanza kuchunguza,” imesema taarifa hiyo.

“Jeshi la Polisi lingependa kutoa tahadhari tena kwa mara nyingine kwa Watanzania, kwani kama mtakumbuka tahadhari zilishawahi kutolewa kuanzia sakata la kampuni zingine ambazo ziliwahi kujinasibu kutoa huduma kama hizo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages