Breaking

Tuesday, 11 October 2022

MLINZI WA KANISA ATOWEKA NA MILLIONI 29 ZA SADAKA



Makasisi na waumini wa Kanisa la ACK All Saints Mountain View wamepigwa na butwaa baada ya mlinzi wao anayeaminiwa zaidi kuiba KSh 1.5 milioni ( millioni 29 za Tanzania)

Kanisa hilo lililopo Kangemi Nchini Kenya, lilikuwa limechangisha pesa hizo kusaidia katika maendeleo lakini mipango yao iliharibiwa na mlinzi huyo ambaye alivunja hazina ya kanisa kabla ya kutoweka.

Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya, mshukiwa huyo anadaiwa kuiba fedha hizo kutoka kwa madhabahu ya kanisa hilo.

“Wakati mzee wa kanisa John Wainanina na mweka hazina Elizabeth Njoki walipokwenda kanisani kuchukua pesa hizo leo asubuhi, walikuta milango ikiwa wazi, jambo ambalo sio la kawaida."

"Walipotazama kwa makini meza ya Bwana ambapo mkate na divai huwekwa, walishtuka kupata ikiwa imevurugwa na pesa zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye droo chini ya madhabahu hazipo!" DCI alisema.

Wazee hao wa kanisa walipiga ripoti kwa polisi ambao wameanzisha uchunguzi wa kumsaka mshukiwa.

Waumini wa kanisa hilo ambao walighadhabishwa na wizi huo walisikika wakitoa laana kwa mshukiwa huku wengine wakimtaka asamehewe iwapo atajitokeza na kutubu dhambi zake.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages