Breaking

Friday, 14 October 2022

MBIO ZA BAISKELI ZAFANA TABORA, WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA MICHEZO



Na Lucas Raphael,Tabora

Afisa Michezo Mkoa wa Tabora, Katuli Hassani amewamasisha wananchi kutumia fursa za michezo ili kuinua uchumi na kujenga afya zao.

Kauli hiyo ilitolewa leo Ijumaa Oktoba 14, 2022 kwenye viwanja vya Alli Hassani Mwinyi wakati akizindua michezo ya mbio za baiskeli kuadhimisha siku ya kumbukizi ya Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere .

Afisa michezo huyo alisema kwamba wananchi watumie fursa za michezo mbalimbali inayofanyika mkoani hapa.

Maadhimisho hayo alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batrida Buriani ambaye alisema kwamba wananchi wanapaswa kujitokeza kwenye mazoezi mara kwa mara ili kunenga afya zao.

Aidha alisema katika kuadhimisha kumbukizi hiyo kupitia michezo mbalimbali ilifanyika ya mashindano ya baiskeli, mbio za kawaida na kiweza kupata washindi kutoka mkoani hapa.

Aliwataja washindi hao wa baiskeli kundi (a) Masunga Mrisho, (b) Rajabu Issa (c) Samweli Mussa ambapo kwa sasa waliweza kuchuja na kupata mmoja ambaye atakaye wakilisha mkoa wa Tabora.

Mashindano mengine ya mbio za kawaida kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoani hapa walioshinda mita 100 Frendnard Lucas,Evodia Nasibu na Haruna Nasibu na wengine mita 4oo Jombo Hamisi, Evodia Nicas na mita 1,500 Mrisho Gambo, Masesa Juma na Bahati Dua.

Kwa upande wake mratibu wa chama cha Riadha mkoani Tabora Allan Ntana alisema kuadhimisha kumbukizi la hayati Mwali Julius Kambarage Nyerere ni kumkumbuka kwa jinsi alivyokuwa akipenda michezo ya aina mbalimbali ndani ya nchi na nje.

Alisema hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni muwaasisi na alikuwa anaipigania nchi yetu enzi ya Uhuru na mwana michezo.

Aidha Ntana alisema kwamba aliwapenda wananchi waliokuwa wakipenda mchezo wa jadi wa bado na kushiriki kwa wananchi katika mchezo huo.

Hata hivyo alisema hayati Mwalimj Julius Kambarage Nyerere alikuwa hapendi ubaguzi wa rangi wala kabila aliwapenda wananchi wake.

Amewahimiza vijana mkoani hapa kujitokeza kushiriki michezo mbalimbali ili kujenga afya zao na waweze kujipatia kipato



Mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages