Breaking

Monday, 10 October 2022

EQUITY BANK YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA


Bi Leynnette Machibya(Head of Risk and Compliance) kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Isabela Maganga akihudumia baadhi ya wateja katika uzinguzi wa week ya huduma kwa wateja leo.

******

Na Mwandishi wetu


Benki ya Equity (T) imezindua rasmi wiki ya huduma kwa wateja jijini Dar Es Salaam kwenye tawi lake la Mwenge.


Wiki ya Huduma kwa Wateja ni wiki ambayo huwa inasherehekewa dunia nzima ikiwa na nia ya kushukuru wateja mbalimbali ambao ndio mchango mkubwa kwa maendeleo ya taasisi.


Equity Bank inasherehekea wiki hii kwa kauli mbiu ya kipekee ikisema ‘Karibu Memba, Tujienjoy na huduma’.

‘Mteja kwetu ni zaidi ya familia, ni memba. Tunahakikisha anapata huduma zote stahiki, kwa wakati na kidijitali’ alisema Bi. Leynette Machibya akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Isabela Maganga.



Aliendelea na kusema kuwa Benki yetu imeendelea kuboresha huduma zake na kuhakikisha kuwa inatanua wigo wake wa upatikanaji nchini kama ufunguzi wa tawi letu la Kahama ili kuweza kuwafikia wateja wote Tanzania na kuhakikisha kuwa tunatimiza dhamira yetu ya kubadilisha maisha ya kila Mtanzania.


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja, Bi. Leynette Machibya aliendelea akisema, huduma zetu ni nafuu zaidi nchini na hivyo kuendana na lengo letu la kukomboa Watanzania kiuchumi kwa kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anatumia mifumo rasmi ya kifedha (financial inclusion).


Ni benki pekee isiyo na makato yoyote ya mwezi na makato ya ziada kwenye miamala.



Ameongeza kuwa wana huduma mbalimbali ambazo zinamfikia kila Mtanzania, ambazo zikiwemo kutunza akiba, mikopo ya mtu mmoja mmoja, wakulima, wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo, vikundi, waajiriwa, n.k.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages