Breaking

Thursday, 13 October 2022

MCHUNGAJI ATUHUMIWA KUMBAKA BINTIYE WA MIAKA SITA




Mchungaji Nurdin Abdallah wa kanisa la kilokole lililopo Kisesa Mwanza amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Magu jijini humo kwa kosa la kumbaka mtoto wake wa miaka sita.

Mchungaji huyo mkazi wa Kisesa, amefikishwa Mahakamani Jumatano ya Oktoba 12, 2022 mbele ya hakimu Mwandamizi wa Wilaya hiyo, Erick Kimaro na kusomewa mashtaka ya kubaka.


Akisoma Mashtaka hayo ya kesi namba 76 ya mwaka 2022, Hakimu Kimaro amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo baada ya kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake ambaye alikuwa mke wa mchungaji huyo kabla ya kuachana.

Mchungaji huyo aliachana na mkewe Julai 2022 na kwenda kuishi Wilaya ya Bunda mkoani Mara huku yeye akibaki kuishi na mtoto wake huyo wa miaka sita ambaye anadaiwa kumuingilia kimwili mara kwa mara.


Majirani waligundua jambo hilo na walipomhoji mtoto huyo aliwathibitishia kuingiliwa na baba yake hivyo kuchukua uamuzi wa kumpeleka mtoto Kituo cha polisi kufungua kesi, na kupewa fomu namba tatu (PF3), akapelekwa hospitalini.


Hata hivyo, mshtakiwa hakuwa mahakamani badala yake aliwakilishwa na mdhamini wake, Bernad Mashauri aliyedai mshtakiwa huyo amevimba sehemu zake za siri ameshindwa kutembea.


Kutokana na hali hiyo, Hakimu Kimaro aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, 2022 huku akimtaka kuhakikisha mshtakiwa huyo afike na vyeti vya hospitali kithibitisha kuumwa kwake.

Source: Mwanachi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages