Breaking

Friday, 7 October 2022

AUNGUZWA KWA UJI NA SHANGAZI YAKE AKIDAIWA KUIBA MAHARAGE JIKONI



Kijana Elvis Shoo (27) mkazi wa kitongoji cha Bogini Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amelazwa katika kituo cha Afya Pasua akiuguza majeraha ya moto, yaliyotokana na kuunguzwa kwa uji na shangazi yake akidaiwa kuiba maharage jikoni.

Tukio hilo ambalo linadaiwa kutokea Septemba 30 mwaka huu mchana nyumbani kwa bibi yake eneo la Bogini, linadaiwa kusababishwa na mzozo uliotokana na kijana huyo kuchukua maharage bila idhini ya shangazi yake.

Uji huo ulimuunguza kijana huyo na kumsababishia majeraha sehemu za shingoni kuelea kifuani na kulazwa hospitalini ambako anaendelea na matibabu mpaka sasa.

Akizungumza leo Alhamisi Oktoba 6, Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, tukio hilo limeripotiwa kituo cha polisi majengo na anafuatilia ili kupata taarifa kamili.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bogini, Zubery Bakari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa mwanamke anayedaiwa kufanya kosa hilo tayari amekamatwa na polisi.

"Ilikuwa ni siku ya Ijumaa, nilipata simu kwa mtu nisiyemfahamu na nilipomuuliza alijitambulisha kuwa anaitwa Elvis, ndipo akanieleza amemwagiwa uji na shangazi yake ameungua na tayari amepitia polisi na wakati huo alikuwa akienda Hospitali..

Soma Zaidi Hapa >>>MWANANCHI <<<

Source: Mwanachi 
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages