Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, linawashikiliwa watu wawili kwa tuhuma za mauaji wa mwanafunzi wa shule ya msingi Mtumba, Farida Makuya (16).
Mwanafunzi huyo aliuawa usiku wa juzi Jumanne, Oktoba 4, 2022 nyumbani kwao Mtumba jijini Dodoma na watu wasiojulika.
Inadaiwa alipigwa na kitu kizito kichwani wakati mama yake akifanya biashara katika klabu cha pombe.
Farida alitakiwa kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi iliyoanza jana na kutarajiwa kumalizika leo Alhamisi ambapo mwili wake ulizikwa jana katika makaburi ya Mtumba na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa jiji la Dodoma.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma (RPC), Martin Otieno amesema hadi leo Alhamisi Oktoba 6, 2022, jeshi hilo linawashikilia watu wawili kwa mahojiano lakini msako zaidi unafanyika.
Otieno amesema tukio hilo ni baya ambalo haliwezi kuvulimika kwani kitendo kilichofanyika kwa binti huyo ni cha kinyama kinachopaswa kulaaniwa.
"Kwa sasa tumewakamata watu wawili kwa mahojiano, tunaendelea na msako mkali, kwa kitendo hiki lazima wahusika wakamatwe na watiwe mbaroni, lakini hili ni tukio baya, baya, baya sana lazima tushughulike nao," amesema Otieno.

Source: Mwananchi