Breaking

Monday, 31 October 2022

MAMA AMUUA MWANAE MCHANGA, AWEKA MWILI NDANI YA NDOO



Polisi katika kaunti ya Kajiado, wamemkamata na kumzuilia mwanamke mwenye umri wa miaka 34, ambaye anatuhumiwa kumuua mwanawe mchanga na kutupa mwili wake nyumbani kwa zaidi ya miezi mitatu.

Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi na bintiye mama huyo mwenye umri wa miaka 14, ambaye alilalamika kuwa nyumba yao iliyoko kwenye mtaa wa mabanda wa Majengo ilikuwa inatoa uvundo mkali.

Baada ya kukagua nyumba hiyo, maafisa wa polisi walipata mabaki ya mtoto huyo ndani ya ndoo ya plastiki chini ya kitanda.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa polisi wa Kaunti Ndogo ya Kajiado Daudi Loronyokwe alisema mwanamke huyo atafikishwa mahakamani Jumatatu, Oktoba 31, huku polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo la kustaajabisha.

Loronyokwe aliwataka wazazi kutafuta msaada wakati hawana uwezo wa kushughulikia masuala ya watoto wao badala ya kufanya vitendo hivyo vya kinyama.

Pia imebainika kwamba mama huyo alijifungua katika hospitali moja mjini humo mnamo Julai 16, 2022.

Maafisa wa upelelezi pia wanatazimwa kupima afya ya kiakili ya mwanamke huyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages