Mwanamke Mmoja mwenye umri wa Miaka 34, mkazi wa Mwamala kijiji cha Igumangobo Kata ya Idukilo Tarafa ya Mondo Wilaya ya Kishapu Mkoa Shinyanga, Getruda Paul ameuawa na mumewe George Mahona mwenye umri wa miaka 38 kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kifuani na shingoni) chanzo kikitajwa wivu wa kimapenzi.
Mauaji hayo yametokea jana Oktoba 19, 2022 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika kijiji cha Igumangobo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga, ACP Leornard Nyandahu amesema Mwanamke huyo Getruda Paul ameuawa na mume wake, George Mahona kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kisha mwanaume huyo Kujiua kwa kujinyonga chumbani kwao.
”Majira ya saa 1 asubuhi, Jana tulipata taarifa ya Tukio la mauaji ya Getruda Paul, ,aliyeuawa na George Mahona, ambaye ni Mumewe kwa kumtuhumu mkewe kuchepuka na mwanaume mwingine ambapo bado hajajulikana, mara baada ya kufanya mauaji hayo, Mtuhumiwa huyo alichukua jukumu la kujiua kwa kujinyonga na kamba ya chandarua”Amesema Nyandahu.
“Miili yote ilifanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Serikali Wilaya Kishapu na miili yote ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu zao kwaajili ya taratibu za mazishi”Ameongeza Nyandahu.
Aidha Nyandahu ametoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi huku akibainisha mpango mkakati wa Jeshi la Polisi kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayevunja sheria huku upelelezi ukiendelea ili kubaini undani wa tukio hilo.
Source: HUHESO DIGITAL