Polisi huko katika maeneo ya Tharaka-Nithi , wanamshikilia mzee mmoja mwenye umri wa miaka 70 akituhumiwa kuwalawiti watoto wawili wa kike wenye umri kati ya miaka 7 na 11 huko katika maeneo ya Kirangare nchini Kenya.
Akithibitisha tukio hilo msaidizi wa polisi eneo la Kirangare Geoffrey Kimbo amesema kwamba mzee huyo ambaye alitiwa nguvuni ijumaa wiki hii anashikiliwa katika kituo cha polisi Marimanti .
Mzee huyo alikua ameajiriwa kwa ajili ya kuchunga ngómbe kwenye nyumba ya waathiriwa.
Watoto hao wa kike ambao baba yao aliwaacha nyumbani na kuelekea Nairobi alishangaa kumkuta mzee huyo akiwa kitandani na binti zake wakiwa uchi .
Watoto hao wamepelekwa kwa daktari ambao ilithibitika kwamba waliingiliwa.
Bw. Kimbo amewaonya wazazi kutowaacha watoto wao na wageni ama ndugu wasiowaamini.
EATV