Breaking

Wednesday, 12 October 2022

AJALI YAUA WATU WATANO, YAJERUHI 30 - MBEYA



Watu watano wamefariki na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu katika Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya jana Jumanne Oktoba 11, 2022 majira ya saa mbili asubuhi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Christina Msyani amesema ajali hiyo imehusisha gari la Kyela Express iliyokuwa inatoka kyela kwenda DSM,coaster iloyokuwa inatoka mbeya kwenda kyela na coaster nyingine iliyotoka DSM kwenda tukuyu kupeleka msiba.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dkt Vincent Anney amesema kuwa madereva wote wawili akiwemo dereva wa Coaster aambaye amefariki, alikuwa akiendesha mwendo kasi na kutaka kulipita lori lililokuwa mbele yake na kusababisha kugongana uso kwa uso na basi la Kyela Express.

"Ajali hii imetokana na uzembe wa madereva ambapo kila dereva alikuwa ana-overtake lori ambalo lilikuwa linapita, na barabra za Rungwe zipo kwenye maeneo ya milima ambapo madereva wanatakiwa kuwa makini,"- Dc Dkt Anney

Naye Mganga Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya Diodes Ngaiza amethibitisha watu watano kufariki huku majeruhi wakifikia 31.

"Vifo vya watu watatu vimeongezeka kutokana na majeruhi 14 waliokimbizwa katika hosptali ya Mission ya Igongwe na hivyo kuongeza idadi ya vifo kutoka watu wawili waliofariki katika eneo la tukio na kufanya idadi ya vifo kuwa vitano” amesema.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages