Breaking

Friday, 21 October 2022

AJALI YAUA, YAJERUHI 33 MOROGORO



Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Alfonce, amefariki dunia na wengine 33 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu kugongana kwa nyuma baada ya gari lililokuwa limetangulia mbele kusimama ghafla katika eneo la Makunganya nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro.

Akieleza chanzo cha ajali hiyo Afisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ahmed Remba, amesema ajali hiyo imesababishwa na lori la mizigo kusimama ghafla ndipo gari lililokuwa nyuma yake aina ya Nissan Mitsubishi lenye namba za usajili T 847 CWN iliyokuwa ikiendeshwa na marehemu Alfonce, kisha basi la abiria kampuni ya BM lenye namba za usajili T 959 DDE nalo kugonga kwa nyuma

"Magari yote matatu yalikuwa yanaelekea uelekeo wa Dodoma yakitokea Dar es Salaam, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kusimama ghafla ndipo dereva wa gari dogo akagonga kwa nyuma lori hilo kisha naye kugongwa kwa nyuma na basi la BM bado hatujajua sababu ya lori hilo kusimamia ghafla, kwa sababu baada ya kutokea ajali dereva alikimbia bila kujali kilichotokea hata namba zake za usajili hazijapatikana" amesema Remba

Via: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages