Breaking

Tuesday, 6 September 2022

KAMATI YA BUNGE MAENDELEO YA JAMII YATEMBELEA JKCI, YAIPONGEZA KAMBI YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO



Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imetembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na kukutana na Wataalamu wa magonjwa ya moyo ya watoto kutoka Saudi Arabia wanaoendesha kambi maalum ya upasuaji bure kwa watoto.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Stanslaus Nyongo (MB) iliambatana pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel na Wajumbe wa Kamati hiyo (Wabunge) waliweza kupatiwa maelezo juu ya zoezi hilo na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Prof. Mohamed Janabi,

Ambapo kambi iliyoanza Septemba 3, mwaka huu na kutarajia kumalizika Septembe 9.2022.

Wataalamu hao wa moyo kwa watoto wanatoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya Kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia ambapo wanashirikiana na Wataalamu wa JKCI katika kambi hiyo,

Aidha, JKCI kupitia kwa Dkt. Winnie Masakuya amesema kuwa wanafanya kambi maalum ya upasuaji wa moyo kwa watoto bure, ambapo ameomba wazazi waweze kuwapeleka watoto wao.

"Tunawaomba wazazi na Madaktari wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo kama;

matundu, mishipa ya damu ya moyo kutokuwa katika mpangilio wake (ASD for device closure, PDA for device closure, BAD, & Pulmonary valvular stenosis) wawalete kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na upasuaji kwa wale itakaolazimika." alisema Dkt.Winnie Masakuya.

Nae Mjumbe wa Kamati hiyo, Ambaye ni Mke wa
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Kikwete aliomba wazazi kutoka mikoa yote kuweza kujitokeza kwa wingi kupeleka watoto wao ilikupatiwa uchunguzi wa moyo, kwani ni fursa ya kipekee uwepo wa Wataalamu hao,
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages