Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Kassim Said ameonyeshwa kukerwa na kundi la wafanya Biashara wanaokiuka maelekezo ya Serikali kwa kuendelea kuuza bidhaa zilizomaliza muda na mifuko ya Plastiki.
Hayo yamekuja wakati wa zoezi la kukagua bidhaa zilizomaliza muda pamoja na Vifungashio vilivyopigwa marufuku na serikali ambapo linafanyika Wilayani Kishapu ambalo limeanza jumatatu september 12, 2022 ambapo september 13 limefanyika katika kata ya Mondo.
Tazama
Katika zoezi hilo la siku mbili jumla ya wafanyabiashara 30 walikamatwa kwa makosa ya kuuza bidhaa zilizoisha muda wake na Mifuko ya blastiki ambapo walitozwa faini.

Kassim ameeleza kuwa wamebaini baadhi ya wafanyabishara bado wanatumia Vifungashio vilivyopigwa marufuku na kuuza bidhaa zilizomaliza muda hali inayohatarisha afya za wananchi wa Kishapu.
"katika operation yetu tunaangalia vitu vyote vinavyohusiana na Usafi, toka tuanze zoezi hili la ukaguzi tumekama bidhaa nyingi zilizomaliza muda pamoja na mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na Serikali" ameeleza
Aidha ametoa rai kwa Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kufuata maelekezo ya serikali na kuongeza kuwa watakaokiuka watachukulia hatua za Kisheria.
Kwa Upande wake Bwana Afya wa Wilaya ya Kishapu Daniel Madaha ameeleza kuwa kabla ya kufanyika ukaguzi huo elimu ilitolewa kwa wafanyabiashara juu ya kutouza Mifuko ya plastiki na bidhaa zilizoisha muda wake.
"tukiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kishapu Ndgu Emmanuel Johnson amepita katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kishapu na kutoa maelekezo na kutoa muda ifikapo tarehe 12.09.2022 mifuko yote ya plastiki na bidhaa zilizomaliza muda wake zisionekane ndani ya wilaya yetu kwa hiyo sisi Tupo katika utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Serikali" ameeleza
Pia katika zoezi hili tumekusanya mifuko ya plastiki na bidhaa ambazo hazina Ubora hivyo tunasubiri kupewa utaratibu na mamlaka kwa ajili ya uteketezaji wa bidhaa hizo sisi kama Maafisa Afya tutahakikisha tunaelimisha jamii na kutokomeza kabisa mifuko hii ya plastiki na kuwaelekeza wafanya Biashara kuhusu Ubora wa bidhaa wanazotakiwa kuziuza" alisema Madaha