Breaking

Thursday, 8 September 2022

CCM YAITAKA SERIKALI KUSIKILIZA MAONI YA WANANCHI KUHUSU TOZO



Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana katika kikao chake maalum Jana September 07, 2022 chini ya Mwenyekiti CCM na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Dar es salaam ambapo imeielekeza Serikali kutazama hali halisi na kuchukua hatua stahiki kuhusu ushauri na maoni ya Wananchi kuhusu tozo.

Akizungumza na Wanahabari Dar es salaam leo Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa-Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imepokea, kutafakari na kujadili kwa kina kuhusu hatua za kibajeti zinazoendelea kuchukuliwa kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo kwa kasi ili kuwawekea wananchi mazingira mazuri ya kujipatia maendeleo.

“Eneo moja wapo ikiwa ni kupitia tozo ambapo ni ukweli usiopingika kwamba Serikali imeweza kufanya mambo makubwa katika kipindi kifupi kwa mfano; kama vile ujenzi wa Vituo vya Afya 234 na Shule mpya za Sekondari 214 na maeneo mengine kadhaa ambayo yanagusa maisha ya watanzania ya kila siku”

“Hata hivyo baada ya kutafakari na kujadiliana kwa kina Kamati Kuu imeona umuhimu wa Serikali kusikiliza maoni na ushauri wa Wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti hiyo, hususani katika eneo la tozo za miamala ya kielektroniki, iliyoanza kutekelezwa hivi karibuni
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages