Breaking

Monday, 12 September 2022

DC MKUDE AKERWA NA UTORO WA WANAFUNZI KISHAPU, ATOA MAAGIZO MAZITO



Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude Ameagiza wanafunzi wote watoro katika Shule ya Sekondari Ng'wanima kurejea Shule mara moja kabla ya Tarehe 14. 09.2022

Maagizo hayo ameyatoa leo September 12, 2002 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza shuleni hapo na kukutana na Uongozi Pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo iliyopo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

Dc Mkude ameeleza kuwa kiwango cha utoro wa wanafunzi shuleni hapo ni kikubwa hivyo kuwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kuhudhuria shuleni Jumatano kabla hawajachukuliwa hatua kali za kisheria.

"kwa Takwimu za Mkuu wa Shule ananiambia walipaswa kuwa wanafunzi 248 leo nakuta wanafunzi 170 kama 78 hawapo, kiwango hiki cha Utoro ni kikubwa , majengo haya Mazuri yaliyojengwa na Rais Samia Suluhu Hassan Mnataka ayakalie nani?" Ameeleza Dc Mkude

"sasa nawatuma kupeleka salamu kwa watolo wote na wazazi wao awe na uniform asiwe na Uniform kurejea Shuleni Mara moja kabla ya Hatua kali za Kisheria kuchukuliwa dhidi yao" amesisitiza

Dc Mkude Ametoa onyo kali kwa Wazazi Ambao wanatabia za kuwaachisha masomo watoto wao kwa ajili ya kuwaozesha tabia hizo waache mara Moja.

Aidha Mkuu wa Wilaya amemuagiza Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu ASP. Joseph Buyuya Baada ya tar 14 .09.2022 kwa watoro wote Ambao watakuwa bado hawajarejea Shuleni kufanya msako wa Nyumba kwa Nyumba Mzazi na mtoto wote wataajibika.

Kwa Upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Ng'wanima Bwana Juma Kihamaya amekili kuwepo na watoro sugu 78 ambao Tayali alishawandikia Barua wazazi wao za Kuwataka wafike Shuleni kwa kusudio la kutoa maelezo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages