Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeridhia kufuta tozo za miamala ya Benki.
Waziri Nchemba ameeleza hayo Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho hayo yataanza kutumika kuanzia October 1, 2022.
Marekebisho aliyoyataja ni pamoja na Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka Benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya Benki moja (pande zote) na Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka Benki moja kwenda Benki nyingine (pande zote).
Aidha Mwigulu ameeleza kuwa Serikali imesamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa Benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.
“Ikumbukwe kuwa tozo hizo ambapo viwango vya tozo vilishushwa kwa asilimia 30 kutoka kiwango cha juu cha shilingi 10,000 hadi kiwango cha juu cha shilingi 7,000, viwango ambavyo vilianza kutumika tarehe 07 Septemba, 2021”
“Kadhalika, Rais alisisitiza alisisitiza kupunguzwa zaidi tozo ambapo Wizara ya Fedha ilipunguza tozo zaidi kwa kushusha tena kiwango cha juu kutoka 7,000 hadi 4,000”
Mabadiliko mengine aliyoyataja ni pamoja na Wafanyabiashara (merchants) kutohusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa.