Wakazi wa Kijiji cha Igawa, Malinyi mkoani Morogoro, wameiomba serikali wilayani hapo kuwasaidia kwa kile kinachodaiwa kuwepo kwa popo bawa anayewaingilia watoto wa kike na wake za watu nyakati za usiku, na kwamba wanahofu ya kupata magonjwa ikiwemo VVU.
Wananchi hao wamedai popobawa huyo alikuwa anatumia imani za kishirikina ndipo aingie ndani ya nyumba na kutekeleza matukio hayo.
Hali hiyo imemlazimu Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mathayo Masele, kufika kwenye Kitongoji hicho na kukutana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo, na kusema kwamba Popobaya huyo amepelekea wanaume wasiheshimike ndani ya ndoa zao kwani imefikia hatua wakiamka wanakuta wake zao wameshaingiliwa.
Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Sungu Sungu kitongoji cha Igoloka Pius Mbala amesema sungusungu kwenye kitongoji hicho wamefanikiwa kumkamata popobawa huyo ambaye anatuhumiwa kufanya matukio hayo pia ni binadamu mwanumume na jina lake limehifadhiwa.
Kutokana na changamoto hiyo Mkuu wa wilaya ya Malinyi akizungumza na wakazi wa kitongoji hicho baada ya kufika mara moja katika eneo hilo, amewaomba wakazi hao kuwa watulivu na kwamba Jeshi la Polisi linafuatilia ukweli wa taarifa hizo.
Source: EATV