Breaking

Thursday, 22 September 2022

MTOTO WA MIAKA MINNE AUAWA NA SHANGAZI YAKE, AMUWEKA KWENYE BESENI NA KUMTUPA PEMBEZONI MWA MTO



Mtoto aliyetambuliwa kwa jina la Enock Melita (4) mkazi wa kijiji cha Kiru Six kitongoji cha Ndoroboni wilayani Babati mkoa wa Manyara ameuwawa kikatili na shangazi yake anayejulikana kwa jina la Nembris Melita na kisha kumbeba na beseni la kufulia nguo na kumtupa pembezoni mwa mto

Mama mzazi wa mtoto huyo Upendo Lendoya amesema mtoto wake ameuawa na wifi yake na hana la kufanya anatafakari kilichotokea.

Wakazi wa kijiji hicho wamegoma chakula kupikwa kwenye msiba huo kutokana na mauwaji ya kikatili yaliyofanyika kwa mototo huyo na kutokuwa na ushirikiano wa ndugu wa marehemu

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amesema uchunguzi bado unaendelea na pindi utakapo kamilika mtuhumiwa atapewa haki yake huku mwakilishi wa dawati la jinsia akihamasisha Amani itawale kwenye kijiji hicho hadi upelelezi ukamilike.


Source: EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages