Breaking

Wednesday, 7 September 2022

CHELSEA YAMTEMA KOCHA TUCHEL



Na Said Muhibu, LLH

Klabu ya Chelsea imefikia makubaliano ya kuachana na Kocha Mkuu wa timu hiyo Thomas Tuchel baada ya kuwa na muendelezo usioridhisha ndani ya klabu hiyo.

Klabu hiyo iliyo chini ya umiliki wa Mfanyabiashara wa Marekani na mmiliki wa kampuni ya Eldridge Todd Boehly na Cleaverlake imetoa taarifa juu ya kufikia makubaliano na Tuchel kuacha kuinoa klabu ya Chelsea.

"Wakufunzi wa Chelsea watasimamia timu kwa mazoezi na maandalizi ya mechi zetu zijazo huku Klabu ikipiga hatua kwa haraka kuteua kocha mkuu mpya," ilisema taarifa hiyo.

Raia huyo wa Ujerumani alirithi mikoba ya kuinoa Chelsea kutoka kwa Frank Lampard mwanzoni mwa mwaka 2021 huku akitwaa mataji makubwa barani ulaya ikiwepo Klabu bingwa barani Ulaya akiwa kocha wa pili kutwaa taji hilo baada ya kocha Roberto Di Mateo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages