Breaking

Tuesday, 6 September 2022

MGODI WA ALMASI WA WILLIAMSON DIAMOND WASAINI MKATABA WA BILIONI 1.2 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO KISHAPU

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude (wa kwanza kushoto) wapili ni Wakili na Mwanasheria wa Mgodi huo Sylivia Leonidas, Meneja mahusiano ya jamii wa Mgodi Bernard Mihayo akimuwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu William Jijimya, na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Matinyi wakionesha hati za makubaliano. (picha zote na Samir Salum)

*********

Na Samir Salum, Lango la habari

Mgodi wa Almasi wa Mwadui Williamson Diamond Ltd uliopo katika Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Umesaini rasmi Mkataba wa Bilioni 1.2 (1200,000,000) wa huduma za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kata tano zinazozunguuka mgodi huo.

Mkataba huo umesainiwa leo Jumanne September 06, 2022 baina ya Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Matinyi na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo William Jijimya .

Upande wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd ukiwakilishwa na Meneja mahusiano ya jamii wa Mgodi Bernard Mihayo Akisaini kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu pamoja na Wakili na Mwanasheria wa Mgodi huo Sylivia Leonidas ukishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude.



Akielezea juu ya mkataba huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Matinyi kwa sasa mkataba huo una manufaa makubwa kwa halamshauri na wananchi kwani awali mgodi ulikuwa ukitoa milioni 156 kwa mwaka hali iliyopelekea kusuasua kwa miradi ya maendeleo kwenye kata zinazozunguuka mgodi huo.



Amesema kwa mwaka huu wa fedha 2022/23 mgodi utatoa shilingi Bilioni 1.2 ambazo zitaenda kutekeleza miradi 18 kuanzia ngazi za vijiji, kata hadi wilaya ambapo pia zitatekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo kuendeleza ujenzi wa Stendi ya Maganzo ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri.

“fedha hizi zitaenda kutekeleza miradi ya aina tatu, tutakuwa na miradi kuanzia ngazi ya vijiji, miradi ngazi za kata mfano katika kata ya ibukilo kutakuwa na mradi wa kuendeleza kituo cha afya, asilimia 20 za fesha zitaenda kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo kuendeleza stendi yetu ya maganzo"Amesema


Kwa upande wao wawakilishi wa mgodi wa Williamson Diamond Ltd Meneja mahusiano ya jamii wa Mgodi Bernard Mihayo akimuwakilisha Mkurugenzi Mkuu pamoja na Wakili na Mwanasheria wa Mgodi huo Sylivia Leonidas wamesema kuwa mkataba huo ushirikishwaji wa wananchi kwenye maeneo husika kwa mahitaji yao ya msingi pamoja na viongozi wa Halmashauri na kuelezea kuwa mabadiliko hayo na mazungumzo ya pande zote mbili na kufikia tamati ya makubaliano ya kutekeleza miradi hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude ameutaka uongozi wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd kutekeleza Makubaliano hayo kwa wakati huku akiwataka viongozi wa Halmashauri kuwa baada ya kupokea fedha hizo kutakiwa kutekeleza miradi husika kwa uaminifu na ionekane kwa jamii ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

“miradi itekelezwe kwa uaminifu na ionekane kwa jamii, madiwani ambao mnazunguuka mgodi ni jukumu lenu kuhakikisha miradi hiyo inaonekana, niwashukuru pia kwa kuanzisha miradi ya kimkakati ambayo itaongeza mapato ya Halmashauri” amesema Dc Mkude



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu William Jijimya ameushukuru Mgodi wa Williamson Diamond Ltd huku akiahidi kuwa fedha hizo zitasimiwa vizuri ili ziweze kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages