Breaking

Thursday, 15 September 2022

MKE AJINYONGA AKITUHUMIWA NA MUMEWE KUIBA ELFU KUMI



Mkazi wa Kijiji cha Nyarututu, kata ya Bwanga wilayani Chato Mkoa wa Geita Asia Kibishe (27) anadaiwa kujinyonga kwa kipande cha kanga kutokana na mumewe kumtuhumu kuiba Sh 10,000 zilizokuwa chumbani kwao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Mwanamke huyo alijinyonga na kipande cha kanga hadi kufa.

Kamanda amesema mwili wa mwanamke huyo umekutwa ukining'inia kwenye mti ulio karibu na nyumbani kwao na chanzo cha tukio hilo ni mgogoro kati yake na mumewe Fabian Shija (23) Mkazi wa Nyarututu.

Amesema mwanamke huyo baada ya kutuhumiwa kuiba Sh 10,000 kitendo hicho kilimkasirisha na kuamua kujinyonga.


Source: Mwananchi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages