Watu watatu wameangamia katika ajali mbaya ya barabarani eneo la Loitoktok baada ya pikipiki mbili kugongana.
Watatu hao waliangamia baada ya kugongana ana kwa ana kwa pikipiki zao walizokuwa wakiendesha.
Chanzo: UGC
Waendeshaji wawili waliaga dunia eneo la ajali huku abiria aliyekuwa amebebwa kwenye bodaboda moja akiaga dunia akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Loitoktok.
Abiria wa pili alipata majeraha mabaya na amelazwa hospitalini ambako anaendelea kupata matibabu.
Kamanda wa polisi wa Loitoktok Shadrack Ruto alithibitisha ajali hiyo ya Ijumaa, Septemba 16, 2022 mwendo wa saa mbili usiku.
“Waendeshaji wanashukiwa kuwa kwenye mwendo wa kasi sana walipogongana,” Ruto alisema.
Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, wahusika wanakisiwa kuwa raia wa taifa jirani la Tanzania kwa kuwa nambari za usajili za pikipiki hizo ni za taifa hilo.
Rais Ruto alihimiza uangalifi barabarani huku miili ya waliofariki ikipelekwa katika makafani ya Hospitali ya Loitoktok.