Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Fatuma Omary Latu, dereva wake na utingo wa Lori wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea leo Septemba 14, 2022 katika eneo la Shamwengo, Inyala mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo vya watu watatu.
Ajali hiyo imehusisha magari matatu ambapo gari kubwa la mizigo lilifeli breki na kugonga magari mengine mawili katika mteremko wa pipe line Kijiji Cha Shamwengo Kata Inyala Mkoani humo.
Mkurugenzi huyo alikuwa anatoka kwenye mkutano mkuu wa 36 wa ALAT uliofanyika jijini Mbeya.
Taarifa zaidi kukujia hivi punde