Breaking

Friday, 2 September 2022

MFANYAKAZI TANESCO AFARIKI BAADA YA KUNASWA NA UMEME



Mfanyakazi wa Shirika la Umeme (TANESCO) mkoani Songwe, amefariki dunia mara baada ya kunasa kwenye nguzo ya umeme wakati akitekeleza majukumu yake katika soko la Malindi lililopo Kijiji cha Isongole wilayani Ileje mkoani humo.

Wakielezea namna tukio hilo lilivyojiri na kupelekea kifo cha George Mwangomola, baadhi ya mashuhuda wamesema kwamba walishtuka tu akiwa juu kumuona akilia na kuomba msaada na hata mwenzake alipotaka kumsaidia ilishindikana na alianguka chini.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Ileje, kwa masikitiko makubwa amesema mfanyakazi wao huyo amefariki wakati akitimiza majukumu yake.

Mwili wa George Mwangomola umesafirishwa na kuzikwa hapo jana katika Kijiji cha Mawengi wilayani Ludewa mkoani Iringa na ametumikia katika shirika la TANESCO kwa muda wa miezi 9 pekee.

SOURCE - EATV
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages