Jeshi la Polisi mkoani Geita linaendelea kumsaka Mashaka Jeremia (40) mkazi wa Lukirini, Kata ya Kalangalala kwa kitendo cha kumuua mkewe Amina Idd (34) kwa kumchoma na kisu kumsababishia majeraha makali yaliyopelekea kifo chake.
Akizungumzia tukio hilo leo September 02, 2022 Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Geita, ACP Ally Kitumbu amesema tukio hilo lilitokea Augusti 30, 2022 majira ya saa saa tano usiku nyumbani kwake Mtaa wa mkoani.
"Amejeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za tumboni, ubavuni na mkononi na Mume wake ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na kwa bahati mbaya alifariki dunia”
Kamanda Kitumbu amesema Mtoto wao Debora Mashaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye ni Mtoto wa marehemu alikuwa akishuhudia tukio hilo na kueleza kuwa Baba ake baada ya kutenda hilo kosa alikimbilia kusikojulikana.
amesema juhudi za kumsaka Mtuhumiwa huyo zinaendelea na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya Geita.
Kwa upande wake Mganga mfawidhi hospitali ya mkoa wa Geita, Dk Mfaume Salum amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambapo amesema mnamo Agosti 31, 2022 saa sita usiku walimpokea Amina akiwa na majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake yaliyosababishwa na kitu chenye ncha kali.
"Mama huyu baada ya kupokelewa alikua anamajeraha sehemu za mwili hasa tumboni na tulibaini yameleta madhara katika viungo vilivyoko ndani ya tumbo tulimfanyia upasuaji usiku huo huo na baada ya kutoka kwenye chumba cha upasuaji baada ya masaa 20 alifariki," amesema Dk Salum.