Breaking

Wednesday, 7 September 2022

DAWA ZA MALARIA, ARV NA KIFUA KIKUU ZINATOLEWA BURE



Na Englibert Kayombo WAF - Kibaha, Pwani

Serikali kwa kushirikiana na Global Fund bado zinaendela kukabiliana na magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kwa kuhakikisha matibabu ya magonjwa hayo yanapatikana bure na kwa urahisi katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afy Ummy Mwalimu akiwa na mgeni wake Bw. Peter Sands Mtendaji Mkuu wa Global Fund walipotembelea Zahanati ya Disunyara iliyopo Wilaya ya Kibaha kuona hali ya utoaji huduma na utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya magonjwa hayo

Waziri Ummy ameishukuru Global fund kwa kuendelea kufadhili upatikaji bure wa dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARV), vipimo vya haraka vya utambuzi wa ugonjwa wa Malaria, Sindano za Malaria kali, Dawa za Malaria (ARU) pamoja na tiba ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.

Hata hivyo Waziri Ummy amewatahadharisha wachanchi kuepuka kununua dawa, vipimo, sindano za Malaria kali kwa kuwa zinatolewa bure ikiwemo pamoja na tiba ya Kifua Kikuu na Ukimwi.

Waziri Ummy ameshukuru Global Fund kwa kuipatia Tanzania zaidi ya Shiligi. Trilioni 1.5 ndani ya kipindi cha miaka mitatu toka 2020 kwa ajili ya utekelezaji wa afua za mapambano dhidi ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria huku pia wakitoa mchango kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 pamoja na kuimarisha mifumo ya afya.

Kwa upande wake Bw. Peter Sands ameshukuru kwa kupata Mwaliko kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuja nchini na kuona namna Tanzania inavyopambana kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria.

“Kwa pamoja tumeweza kupata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya magonjwa haya matatu na kuweza kuokoa maisha ya watu na kupunguza kiwango cha maambuki katika magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria, bado tuna kazi kubwa sana lakini tumepiga hatua kubwa” amesema Bw. Sands

Amesema kuwa hivi karibuni Rais wa Marekani Mhe. Joe Biden anatarajia kufanya Mkutano kwa ajili ya kuhamasisha upatikanaji wa Shilingi Bilioni 18 (USD) Dola za Marekani kwa ajili ya kutunisha mfuko wa Global Fund kuwezesha utekezaji wa mapambano zaidi ya magonjwa hayo
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages