Breaking

Thursday, 11 August 2022

WAFUGAJI , WAVUVI WATAKIWA KUONGEZA MATUMIZI YA ZANA BORA NA MBEGU BORA ZA MAZAO



Na Lucas Raphael,Tabora

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka Wakulima, wafugaji na wavuvi kuongeza matumizi ya zana bora na mbegu bora za mazao,ufugaji wa samaki unaozingatia mbinu za kisasa ili kuongeza tija .

Wito huo umetolewa leo wakati wa kuhitimisha maonesho ya sikukuu ya wakulima nanenane kanda ya magharibi katika viwanja vya maonesho ipuli mkoani Tabora .

Andengenye alisema kwamba wakulima na wafugaji wanapaswa kutumia mbegu bora na zana zilizo bora za kilimo ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi katika kanda hiyo

Aidha aliendelea kusisitiza kwamba ufugaji wa samaki unaendelea kuongezeka kwa kasi katika Kanda ya Magharibi lakini bado idadi kubwa ya wananchi hawajatumia ipasavyo fursa ya uwepo wa Kituo cha Viumbemaji cha Mwamapuli wilayani Igunga mkoani hapa.

Mkuu huyo wa mkoa alisema lengo la kituo hicho cha kanda ni kutoa vifaranga bora vya samaki na elimu kuhusu ya njia bora za ufugaji samaki kwa wananchi .

Naye mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa kigoma alimweleza kwamba Kuna fursa kadhaa za masoko ya mazao yatokanayo na kilimo, mifugo na uvuvi katika Kanda ya magharibi ambayo haitumiki vema.



Alisema kwamba iwapo Fulsa hiyo ikitumika vema itasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya masoko ya bidhaa za wananchi na kitu cha msingi ni kuongeza thamani ya bidhaa hizo.

“Nina amini hatujatumia ipasavyo fursa ya uwepo wa masoko kutoka kwenye nchi tunazopakana nazo kama Congo DRC, Burundi, Rwanda na Zambia.” Balozi Dkt. Batilda Burian

Awali Afisa malisho kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Emmanuel Kato alisema kwamba halmashauri nyingi nchini hazijatenga maeneo kwa ajili ya malisho ya mifugo na badala yake maeneo ya vijiji ndio yanatumika kwa makazi na kilimo .

Alisema jambo hilo ndilo linalosababisha kutomalizika kwa migorogoro baina ya wafugaji na wakulima kwa sababu ya wafugaji kulishia kwenye mashamba ya wakulima .

Aidha alitoa rai kwa wafugaji kushirikia katika zoezi la uwekaji wa hereni kwenye mifugo yao.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Mwaka huu wa 2022 inasema: “Ajenda 10/30 Kilimo ni biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango bora ya kilimo, mifugo na uvuvi “

mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages