Breaking

Wednesday 3 August 2022

KATAVI, MANYARA ZAIBUKA KIDEDEA MCHEZO WA WAVU – UMITASHUMTA



OR - TAMISEMI

Mchezo wa mpira wa wavu kundi D uliochezwa tarehe 3 Agosti 2022 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Tabora, kwa upande wa wavulana Katavi iliishinda Dodoma kwa seti 3-2 huku Kilimanjaro ikipoteza kwa Manyara Seti 0-3 kwa upande wa wasichana.

Mchezo wa Katavi na Dodoma ulichezwa kwa seti tano, ambapo seti ya kwanza ilishudia Dodoma ikipoteza kwa alama 17-25, seti ya pili Dodoma ilijitahidi kurudi mchezoni na kupata alama 25-20.

Kwa upande wa Wasichana Kundi D Manyara iliibuka mshindi dhidi ya Kilimanjaro kwa seti zote tatu.

Mchezo kati ya Kilimanjaro na Manyara ulikuwa wa kusismua wakati wote, huku kila timu ikionesha kujiandaa vema na mashindano ya UMITASHUMTA 2022.

Michuano ya UMITASHUMTA kwa mwaka 2022 yanafanyika kitaifa mkoani Tabora, ambapo mikoa yote ya Tanzania inashiriki kupitia wawakilishi ambao ni wanafunzi wa shule za Msingi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages