Breaking

Monday, 15 August 2022

NAIBU WAZIRI KATAMBI APONGEZA MFUMO WA KUINGIA MIKATABA YA UTENDAJI KAZI NA TAASISI ZA UMMA



Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amepongeza Mfumo wa kuingia Mikataba ya Utendaji Kazi na Taasisi za Umma ambao unaainisha malengo yatakayo tekelezwa na Taasisi za Umma katika kipindi cha mwaka mmoja.

“Mfumo huu una faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwajibikaji katika utekelezaji wa Sera, Mikakati na vipaumbele vya Taasisi za umma na vya kitaifa”

Tunapaswa kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu katika maeneo yetu ya kazi ili kuongeza tija na ufanisi katika kazi tunazozifanya;

Aidha, mshikamano na kufanya kazi kama timu kwa kuwa, Ofisi ya waziri mkuu ndiyo Kioo na Kiongozi kwa Wizara nyingine, hivyo tunatakiwa kuweka usimamizi madhubuti katika Programu, Miradi na kazi zote ambazo zinasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.


Kikao kazi hiki kimehudhuriwa pia na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi ya waziri mkuu ikiwemo Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Pia nimeshuhudia utiaji saini Mikataba ya Utendaji Kazi kwa Mwaka 2022/23 wakati wa kikao kazi cha menejimenti ya ofisi ya waziri mkuu kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages