Breaking

Wednesday, 10 August 2022

RC CHALAMILA AWATAKA WATANZANIA KUJIULIZA MASWALI HAYA KABLA YA KUMLAUMU RAIS SAMIA JUU YA UKOSEFU WA MAFUTA NA MBOLEA NCHINI




Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert John Chalamila amewataka watanzania kuacha habari zenye lawama zinazolenga kuligawa taifa ikiwa ni pamoja na kumlaumu Rais Samia juu ya ukosefu wa mafuta ya petroli pamoja upandaji wa bei ya mbolea nchini.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo Agosti 9, 2022 wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mashujaa Mayunga uliopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

RC Chalamila amesema kuwa sio muda wa kumlauma Rais Samia juu ya ukosefu au upandaji wa mafuta na mbolea badala yake Watanzania wanatakiwa kujiuliza maswali yafuatayo 1: je Mh, Rais wakati anaingia madarakani kuna Rais mstaafu alimkabidhi visima vya mafuta?

Swali la pili je kuna Mkoa gani hapa nchini unazalisha raslimali mafuta?

"Baada ya hapo najua majibu ni hapana ndg zangu naomba kabisa tusitende dhambi ya kumlaumu Rais Samia na katika hili sifanyi siasa uchumi wa mafuta unatoka kwenye mataifa ikiwemo Saudi Arabia na mataifa mengine.

Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa Watanzania wanatakiwa kuacha kumlalamikia Rais juu ya upandaji wa mbolea wakingali wanajua kuwa Rais wakati anaingia madarakani hakukabidhiwa viwanda vya mbolea kwani hadi sasa juhudi zake ni kufikia mwaka 2025 atakuwa amejenga kiwanda kipya.

Hata hivyo amewahimiza wananchi kuacha habari zinazoligawa taifa kwa udini na ukabila.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages