Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu imewasilisha Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Kikao hicho kilihusisha viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene, na Naibu Waziri wake Mhe. Ummy Nderiananga. Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Dkt. John Jingu pamoja na Naibu wake Bwa. Kaspar Mmuya.