Breaking

Thursday, 18 August 2022

NAIBU WAZIRI ULEGA AAGIZA KUKAMATWA MKANDARASI WA UJENZI SOKO LA SAMAKI SENGEREMA



Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega,ameagiza kukamatwa kwa mkandarasi aliyekuwa akitekeleza mradi wa soko la samaki wabichi katika mwalo wa Chifunfu mkoani Mwanza baada ya mradi huo kutokamilika kwa wakati. 

Ulega amesema serikali aitakubali kuona wakandarasi wanakula pesa za kutekeleza miradi ya wananchi hivyo wizara itamchukulia hatua mkandarasi huyo kwa kutoa ripoti bodi ya wakandarasi ili aweze kufungiwa na kuondolewa katika orodha ya wakandarasi nchini.


Aidha ameagiza Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini ( TAKUKURU ) wilayani Sengerema mkoani Mwanza,kumchukulia hatua mkandarasi ambae anatekeleza mradi wa ujenzi wa soko la samaki wabichi katika mwalo wa chifunfu baada ya kuchukua muda mrefu katika utekelezaji wake.

Awali Mbunge wa Jimbo la Sengerema Tabasam Hamis,ameiomba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kumchukulia hatua mkandarasi huyo baada ya kuchelewa kutekeleza ujenzi kwa wakati na serikali ikiwa imelipa zaidi ya sh,milioni 90 kwa ajili ya mradi huo.

Mkandarasi huyo tayari amelipwa zaidi ya sh. milioni 90 ambapo ghalama ya mradi ni shilingi milioni 120.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages